IQNA

Iran yalaani hujuma za kigaidi ndani ya misikiti nchini Afghanistan

10:38 - October 22, 2017
Habari ID: 3471226
TEHRAN (IQNA)- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imelaani hujuma za kigaidi zilizolengamisikiti miwili katika miji ya Kabul na Ghor nchini Afghanistan siku ya Ijumaa na kuuawa waumini zaidi ya 80.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Bahram Qassemi mbali na kueleza masikitiko yake na kutoa mkono wa pole kwa serikali na wananchi wa Afghanistan amesema, magaidi wenye kiu ya damu na wakufurishaji majahili ambao hawaijui hata harufu ya dini na utu, kwa mara nyengine tena wamewaandama kwa mashambulio yao yanayotokana na chukiwananchi madhulumu, wanaoteseka na wasio na hatia wa Afghanistan, lengo lao likiwa ni kuzusha hitilafu za kimadhehebu na kuvuruga amani katika nchi jirani ya Afghanistan.

Watu wasiopungua 80 wakiwemo wanawake na watoto waliuawa Ijumaa na makumi ya wengine walijeruhiwa katika mashambulio ya kigaidi yaliyolenga misikiti miwili katika miji ya Kabul na Ghor nchini Afghanistan. Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) limedai kuhusika na hujuma ndani ya msikiti wa Waislamu wa Jmam Zaman wa Waislamu wa madhehebu ya Shia mjini Kabul huku kundi la Taliban nalo likiaminika kuhusika na jinai katika msikiti wa Ahul Sunna mjini Ghor.  Wakati huo huo magaidi wamehujumu kituo cha kijeshi mjini Kabul Jumamosi na kuwaua wanajeshi 15 waliokuwa hapo. Kundi la kigaidi la Taliban limedai kuhusika na hujuma hiyo. Magaidi wakufurishaji wanatekeleza jinai nchini Afghanistan pamoja na kuwepo wanajeshi wa Marekani na shirika la kijeshi la NATO nchini humo kwa muda wa miaka 16 sasa.

3464221

captcha