IQNA

Kikao cha Kimataifa cha Benki za Kiislamu kufanyika Aprili mjini Istanbul

12:28 - December 17, 2017
Habari ID: 3471313
TEHRAN (IQNA)-Baraza Kuu la Benki na Taasisiza Kifedha za Kiislamu (CIBAFI) limepanga limetangaza kuwa kikao chake cha tatu cha kimataifa kitafnayika Aprili 18-19 mwakani mjini Istanbul, Uturuki.

Kwa mujibu wa taarifa, kikao hicho kitafanyika chini ya kauli mbiu ya, 'Sura Mpya ya Huduma za Kifedha, Vizingiti, Fursa na Masuala Mapya," na kitafanyika kwa hisani ya Halmashauri ya Usimamizi wa Benki nchini Uturuki.

Kikao hicho cha kimataifa cha CIBAFI kinalenga kuwaleta wadau wote katika jukwaa moja kujadili mabadiliko na matukio mapya katika sekta ya kimataifa ya mfumo wa kifedha wa Kiislamu.

Wadau wote wakiwamo wasimamizi, mabenki na wateja wanatazamiwa kufaidika na kikao hicho hasa iwapo watafahamishwa kuhusu masuala kama vile ubunifu ambao utawezesha sekta ya kifedha ya Kiislamu iwe mshindani mkubwa duniani.

Katibu Mkuu wa CIBAFI Abdelilah Belatik, akizungumza kuhusu matayarihi ya kikao hicho amesema: "CIBAFI ina furaha kutangaza kuwa kikao chake cha tatu cha dunia kitafanyika Istanbul Uturuki kujadili maudhui za mfumo wa kifedha wa Kiislamu. Kuna mahitaji mengi na fursa nyingi ambazo hazijatumika. Mufmo wa kifedha wa Kiislamu unaweza kuwa na mchango mkubwa katika ustawi wa kiuchumi na kufunguwa fursa mpya kwa mashirika ya kifedha ya Kiislamu."

3673314/

captcha