IQNA

Njama ya wanazi kuhujumu msikiti Scotland yatibuliwa

19:46 - March 16, 2018
Habari ID: 3471430
TEHRAN (IQNA)- Njama ya watu wenye misimamo mikali ya kinazi ya kuushambulia kwa bomu msikiti Scotland nchini Uingereza imetibuliwa na mshukiwa kukamatwa.

Kwa mujibu wa taarifa Connor Ward, 25, amepatikana na mada zinazoweza kutumika kutegeneza mabomu na kukamatwa. Alifikishwa katika Mahakama Kuu ya Edinburg Jumanne ambapo mahakama imefahamishwa namna alivyopatikana na idadi kubwa ya silaha moto na baridi. Ward aliwahi kufungwa miaka mitatu gerezani mwaka 2012 baada ya kupatikana na mada za miripuko.

Makachero waliofika nyumbani kwake katika eneo la Banff huko Aberdeenshire, wanasema walipata meelfu ya nyaraka za intaneti kuhusu silaha pamoja na propaganda za makundi yenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia. Aidha makachero walipata ramani  za misikiti na vituo tano vya Kiislamu vilivyo mjini Aberdeen, Scoltand. Ward, ambaye aliiambia mahakama kuwa Hilter alifanya makosa kadhaa, alikuwa ameanza kutayarisha kitabu chenye orodha ya misikiti ya Uingereza kwa lengo la kuishambulia.  Ndani ya kitabu hicho kuna sehemu iliyoandikwa hivi: “Kitabu hiki ni maalumu kwa wale wanaomfuata Muhammad na Imani ya Kiislamu. Karibuni hivi mtaangamia”.  Maandishi hayo yalipelekea maafisa wa usalama wafikie natija kuwa Ward alikuwa analenga kutekeleza hujuma za kigaidi. Mahakama inatarajiwa kutoa hukumu yake kuhusu mashtaka yanayomkabili Ward ifikapo Aprili 11 2018.

3700220

captcha