IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Iran imezima njama za kigaidi za Marekani Asia Magharibi

23:53 - March 21, 2018
Habari ID: 3471438
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, katika miaka iliyopita, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeweza kupeperusha bendera ya izza, heshima na uwezo wa kitaifa katika eneo la Asia Magharibi na imekuwa na nafasi muhimu mno katika kuwasambaratisha wakufurishaji na kuleta amani na usalama.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo, katika hotuba yake mbele ya hadhara kubwa ya wafanya ziara na majirani wa Haram toharifu ya Imam Ali bin Mussa al-Ridha AS mjini Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran,  na kusisitiza kwamba, kwa hatua zake Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesambaratisha na kuzima njama za Marekani katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kwamba, hivi sasa madola makubwa ambayo yamekuwa yakiingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine katika maeneo mbalimbali ulimwenguni yamekuwa yakiilalamikia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuhoji kwamba, kwa nini Iran inaingilia masuala ya eneo? Sisi katika kujibu swali hili tuunawaambia kwamba, hilo halikuhusuni.

Ayatullah Khamenei sambamba na kubainisha kwamba, uwepo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika baadhi ya nchi katika Mashariki ya Kati umetimia kwa ombi na matakwa ya nchi husika ameeleza kama nivyomnukuu: Sisi hatujatumia mabavu na wala hatujaingilia masuala ya ndani ya nchi hizo, bali wametaka msaada na sisi tukawasaidia, na msaada huu una msukumo wa kimantiki tena kwa mahesabu ya kiakili na sio kupitia mhemuko na hisia.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria njama na mipango ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi na kusema kuwa, Wamarekani walikuwa wanafuatilia suala la kuzishughulisha na vita nchi za eneo kwa kuyaleta makundi dhalimu na yenye ushari kama Daesh au ISIS, lakini sisi kwa tawfiki ya Mwenyezi Mungu Iran imefanikiwa kusambaratisha njama hiyo.

3701615

captcha