IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Misri yaanza

16:40 - March 24, 2018
Habari ID: 3471442
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya 25 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yameanza leo asubuhi mjini Cairo ambapo yanahudhuriwa na wawakilishi wa nchi 50.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika sherehe za ufunguzi zilihudhuriwa na Sheikh Mohamma Mokhtar Gomaa, Waziri wa Wakfu wa Misri na wageni wengine waalikwa. Akihutubu katika kikao hicho Sheikh Abdul Fatah Al Qussi, mwanachama wa Baraza la Maulamaa wa Misri katika hotuba ya ufunguzi amesema lendo la kuandaa mashindano hayo, ni kuwasilisha taswira sahihi ya Qur'ani na Uislamu kinyume na magaidi wanayotaka kuuchafulia Uislamu na Qur'ani jina.

Mashindano hayo ambayo yataendelea hadi siku ya Alhamisi yanalenga pia kusitiza umoja wa Waislamu katika kuitetea Quds Tukufu.

3701856

captcha