IQNA

Waislamu wawili wauawa kwa kudungwa visu baada ya msikiti kuvamiwa Afrika Kusini

11:11 - June 15, 2018
Habari ID: 3471558
TEHRAN (IQNA)- Waislamu wawili wamethibitishwa kuuawa kwa kudungwa visu wakiwa msikitini katika wakiwa katika Itikaf, baada ya mtu mmoja kuvamia eneo hilo la ibada nchini Afrika Kusini.

Noliyoso Rwexana, msemaji wa polisi katika mkoa wa Western Cape amesema tukio hilo limefanyika Alhamisi alfajiri katika mji wa Malmesbury, ulioko kusini mwa mkoa huo.

Amesema watu wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi hilo na kwamba gaidi aliyehusika na hujuma hiyo pia ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Mmoja kati ya waliouawa katika tukio hilo ametambuliwa kuwa Ismail Bassa aliyekuwa na umri wa miaka 72 na mke wake, Zainab Bassa, amesema mume wake ‘alichinjwa’ wakati alipokuwa akiswali.

Haya yanajiri mwezi mmoja bada ya polisi nchini Afrika Kusini kugundua kifurushi cha mada za milipuko katika msikiti katika mji mdogo wa Verulam nje ya Durban; msikiti ambao juma moja kabla ya hapo ulikuwa umevamiwa na magaidi.

Mei 10, watu wanaosadikiwa kuwa magaidi wakufurishaji waliuvamia msikiti huo wa Imam Hussein AS karibu na mji wa Durban Afrika Kusini na kumuua shahidi Imamu wake kwa kumkata kichwa na kuwajeruhi waumini wengine kadhaa.

Magaidi hao waliokuwa na silaha mbali na kumuua Imamu wa msikiti waliwashambulia waumini kwa kuwadunga visu na kuwajeruhi kadhaa miongoni mwao. 

Hakuna taarifa kuhusu iwapo hujuma hizo mbili zinahusiana na hadi sasa hakuna kundi au mtu yeyote aliyedai kuhusika na mashambulizi hayo ya misikiti ambayo yamepelekea kuenea hofu katika jamii ya Waislamu Afrika Kusini.

3466074

captcha