IQNA

Aplikesheni inayoonyesha migahawa halali Kombe la Dunia Russia

16:54 - June 18, 2018
Habari ID: 3471563
TEHRAN (IQNA)- Kuna idadi kubwa ya Waislamu ambao wako nchini Russia kushiriki au kutazama mechi za Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2018 na moja kati ya changamoto kubwa ni kupata chakula halali, lakini tatizo hilo limetatuliwa kwa kutumie teknolojia ya kisasa.

Waislamu walioko Russia sasa wanaweza kupata migahawa yenye chakula halali kwa kutumia aplikeshni maalumu ya simu za mkononi inayojulikana kama Crave Halal ambayo inapatikana katika App Store.

Mwaka huu kuna nchi saba za Waislamu ambazo zinashiriki katika Kombe la Dunia ambazo ni pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Saudi Arabia, Misri, Morocco, Tunisia, Senegal na Nigeria.  Kwa msingi huo kuna idadi kubwa ya Waislamu waliofika katika kombe la dunia kama wachezaji, maafisa wa serikali, waandishi habari, mashabiki, n.k na wanahitaji huduma za chakula halali.  FIFA inakadiria kuwa kuna mashabiki 100,000 Waislamu waliofika Russia kushangilia timu zao katika Kombe la Dunia nchini Russia ambalo lilianza Juni 14 na linataamiwa kuendelea kwa muda wa mwezi moja.

Nchini Russia idadi ya Waislamu inakadiriwa kuwa milioni 30 na hivyo aplikesheni ya Crave Halal inatazamiwa kuendelea kutumika nchini humo hata baada ya Kombe la Dunia.

"Mashabiki Waislamu wanakumbwa na tatizo kutafuta hoteli nzuri zenye chakula halali na  ni kwa msingi huu ndio tumezindua aplikesheni ya Crave Halal nchini Russia katika Kombe la Dunia mwaka 2018," amesema msemaji wa Crave Halal.

3466102

captcha