IQNA

Manusura wa hujuma ya kigaidi msikitini aliokoka kwa kujificha katika Rafu ya Qur'ani

11:13 - March 17, 2019
1
Habari ID: 3471879
TEHRAN (IQNA) – Pale waumini walipokuwa wakimiminiwa risasi na gaidi wakati wa Sala ya Ijumaa msikitini, dereva wa texi, Abdul Kadir Ababora, alijificha chini ya rafu ambayo hutumika kuweka nakala za Qur'ani Tukufu huku akiomba Duaa kuwa apate fursa ya kubakia na mke na watoto wake.

Uamuzi wake huo wa haraka uliokoa maisha yake, na aliibuka bila jeraha lolote. Alipotembelea eneo  la hujuma hiyo, Jumapili, amesema kunusurika kwake ni kwa ajili ya rehma ya Allah SWT na ni sawa na muujiza. "Wakati nilipoinuka niliona miili ikiwa imetapakaa kushoto na kulia."

Kama, wengi waliokuwa wamefika kwa ajili ya Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al Noor, mjini Christchurch, Ababora alikuwa mhamiaji aliyeingia New Zealand kutoka nchi yake iliyokuwa inakumbwa na misukosuko.

Ababora mwenye umri wa miaka 48 aliwasili New Zealand kutoka Ethiopia mwaka 2010 na wiki mbili zilizopita tu tokea mtoto wake wa pili alizaliwe.

Anasema punde baada ya imamu wa msikiti kuanza kutoa hotuba ya Kiingereza, mlio wa risasi ulisikika nje. Anaongeza kuwa mtu wa kwanza aliyemuona akiwa amepigwa risasi ni mhandisi Mpalestina ambaye pia alikuwa dereva wa texi. "Alisimama kuangalia ni nini kilichokuwa kinajiri na hapo akamuona mshambuliaji. Wakati alipojaribu kukimbia, gaidi huyo alimpiga risasi na akaanguka."

Waislamu wasiopungua 49, wakiwemo wanawake na watoto wadogo, waliuawa katika hujuma za kigaidi zilizofanywa dhidi ya misikiti miwili katika mji wa Christchurch nchini New Zealand wakati waumini wakiwa wamekusanyika kwa ajili ya Sala ya Ijumaa.

Waislamu wengine karibu 50 wamejeruhiwa vibaya katika hujuma hiyo ambayo ilitekelezwa na gaidi raia wa Australia mwenye misimamo mikali ya ubaguzi, Brenton Tarrant, ambaye ni mfuasi sugu wa Rais Donald Trump wa Marekani aliye maarufu kwa misimamo yake dhidi ya Uislamu. Baada ya kugaidi huyo kutekeleza mauaji ya watu 41 katika msikiti wa Al Noor alielekea katika msikiti wa Linwood katika mji huo huo na kuua watu wengine 8.

Ababora anasema wakaazi wengi wa Christchurch hawakuamini jinai kama hiyo ingeweza kujiri mjini humo. Anaongeza kuwa: "Tulikuwa tukisema New Zealand ni eneo salama na tuliuamini mfumo. Waislamu hapa ni watu watulivu, hata misikiti haitangazi adhana kwa vipaza sauti." Hivi sasa New Zealand si eneo salama tena, kuna ukatili mkubwa, amesema Ababora.

3468153

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Mohamed Mbarak Shahbal
0
0
GAIDI HUYO TAARIFA ZAELEZEA KUWA ALITUMWA HILO NA DONALD TRUMP NA NCHI ZOTE DUNIA KOTE ZIMEKILAANI KITENDO HICHO MPAKA SASA LAKINI U S A IPO KIMYA NA BALI VYUO VIKUU KADHAA VIMEKIBARIKI KITENDO HICHO
captcha