IQNA

Dunia yapinga tamko la Trump kuhusu milima ya Golan ya Syria

23:10 - March 24, 2019
Habari ID: 3471887
TEHRAN (IQNA)-Rais Donald Trump wa Marekani amelaani vikali na kutengwa kimataifa kudai kuwa kuwa utawala haramu wa Israel unamiliki miinuko ya Golan ya Syria.

Mnamo Alkhamisi tarehe 21 Machi 2019, rais wa Marekani, Donald Trump aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: "Wakati umefika kwa Israel kuitawalia kikamilifu milima ya Golan. Baada ya kupita miaka 52 sasa wakati umefika kwa Marekani kutambua rasmi kuwa milima ya Golan ni mali ya Israel kwani milima hiyo ina umuhimu mkubwa wa kiistratijia na kiusalama kwa Israel na kwa utulivu wa eneo hilo."

Uamuzi huo Trump usiozingatia sheria za kimataifa katika kujaribu kuutambua rasmi umiliki wa utawala ghasibu Israel kwa miinuko ya Golan ya Syria, umekabiliwa na upinzani mkubwa kutoka nchi mbalimbali za dunia. Mevlüt Çavuşoğlu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki sambamba na kutangaza kwamba nchi yake inaunga mkono umoja wa ardhi yote ya Syria sambamba na kupinga uamuzi huo wa Trump, amesema kuwa, hatua ya rais huyo wa Marekani itashadidisha migogoro katika eneo la Asia Magharibi. Mbali na Uturuki, Umoja wa Ulaya, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Russia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nazo pia zimeonyesha upinzani wao mkali dhidi ya njama ya kutaka kuuhalalisha rasmi udhibiti wa Israel kwa miinuko hiyo.

Maja Kocijančič, msemaji wa Federica Mogherini, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema: Msimamo wetu kuhusu mmiliki wa hii milima ya Golan haujabadilika. Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Umoja wa Ulaya hautambui umiliki wa Israel kwa ardhi ambazo ulizitekwa mwaka 1967 ikiwemo milima ya Golan na sisi hatuitambui milima hiyo kuwa ni sehemu ya Israel.

Pamoja na madai hayo ya Trump, ukweli unabaki kuwa, miinuko ya Golan, ni sehemu isiyoweza kutenganishwa na ardhi ya Syria. Katika vita vya siku sita hapo mwaka 1967, utawala haramu wa Israel na bila kuzingatia sheria, uliikalia kwa mabavu miinuko hiyo ya Golan, ambayo ni milki ya Syria. Kwa kipindi cha miaka 52 sasa utawala wa Israel umefanya juhudi nyingi kwa ajili ya kufanya miinuko hiyo iwe milki yake  na hivyo kuwa sehemu ya ardhi ilizonyakuwa kutoka Palestina.yake.  Lakini si Syria pekee, bali jamii yote ya kimataifa haijakubali katu madai ya Tel Aviv ya kudhibiti miinuko hiyo. Katika uwanja huo azimio nambari 242 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ni miongoni mwa nyaraka muhimu za jamii ya kimataifa ambazo zilitupilia mbali madai ya Israel ya kutaka kujimilikisha miinuko hiyo ya Golan. Azimio hilo linapinga udhibiti wa maeneo yaliyotwaliwa kupitia vita, kama ambavyo Israel nayo iliikalia kwa mabavu miinuko hiyo kupitia vita vya siku sita.

3468181

captcha