IQNA

Hamas utawala wa Kizayuni unalenga kuibua mgogoro Ukanda wa Ghaza

21:32 - August 03, 2020
Habari ID: 3473028
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Harakati ya Muqawama ya Palestina (Hamas) amesema kuwa, utawala wa Kizayuni unatekeleza mashambulizi katika Ukanda wa Ghaza lengo likiwa ni kuwahamishia wananchi wa Palestina migogoro ya ndani ya utawala huo na kupotosha fikra za walimwengu kuhusu matukio na hali mbaya ya kisiasa inayoukabili sasa utawala wa Israel.

Fauz Barhum amesema kuwa wanamuqawama wa Palestina wako macho na wanatambua vyema taswira halisi za njama na mipango ya utawala wa Kizayuni na namna ya kukabiliana na utawala huo. 

Barhum amebainisha haya kufuatia mashambulizi yaliyofanywa jana usiku na utawala wa Kizayuni huko mashariki mwa mji wa Khan Yunis. 

Msemaji wa Hamas ameongeza kuwa, siasa za kukabiliana na adui Mzayuni zitaendelea sambamba na mapambano na jihadi ya wananchi wa Palestina. 

Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni jana usiku zilishambulia eneo la Abu Hadaf mashariki mwa kitongoji cha al Qararah mashariki mwa mji wa Khan Yunis na katika eneo jingine huko Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza. 

Avichay Adraee msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni ametoa taarifa na kudai kuwa, mashambuliz ya jana usiku ya utawala huo ni jibu kwa kitendo cha kuvurumishwa kombora kutoka Ukanda wa Ghaza. Msemaji huyo wa jeshi la Israel ameendelea kudai kuwa, jeshi la utawala huo linaichukulia oparesheni yoyote dhidi ya Tel Aviv kuwa ni hatari na kwamba eti Hamas inahusika na mashambulizi dhidi ya Israel. 

3914308

captcha