IQNA

Wazayuni wapanga 'maandamano ya bendera' dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa, Hamas yatoa onyo kali

16:26 - June 06, 2021
Habari ID: 3473983
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika Ukanda wa Ghaza ametoa tamko baada ya kubainika kuwa Wazayuni wanapanga kutekeleza hujuma nyingine dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds au Jerusalem.

Yahya Sinwar kiongozi wa Hamas katika Ukanda wa Ghaza ameonya kuwa, iwapo Wazayuni watauhujumu tena msikiti wa al Aqsa basi harakati  za muqawama na mapambano zitauharibu mji wa Tel Aviv.

Akizungumza na Shirika la Habari la Palestina la SAFA ameashiria wito wa makundi yenye kufurutu ada ya Israel kuhusu kile ambacho yamekitaja kuwa ni 'maandamano ya bendera' katika mji wa Quds siku ya Alhamisi na kusema: "Iwapo Wazayuni watarejea tena na kuuhujumu Msikiti wa Al Aqsa, sisi pia tutarejea na hilo kwetu halina shaka."

Makundi ya walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali ya kufurutu adha yametoa wito kwa Wazayuni kushiruki katika maandamano ya kichechezo Alhamisi katika Msikiti wa Al Aqsa ambapo gazeti la Kizayuni ya Yedioth Ahronoth limesema Wazayuni hao wanasubiri idhini ya polisi ya utawala haramu wa Israel.

Msemaji wa Hamas Mohammad Hamada naye pia ametoa taarifa  na kuhusu njama hiyo ya Wazayuni ya kuuvamia msikiti wa Al Aqsa ambapo ameuonya utawala wa Kizayuni usijaribu kutoroka kutoka mgogoro wa ndani ya Israel kwa kuibua ghasi mjini Quds.

Aidha amewataka Wapalestina mjini Quds kuchukua hatua za kuulinda na kuuhami Msikiti wa Aqsa siku ya Alhamisi wakati wa hujuma hiyo tarajiwa ya Wazayuni.

3975822

Kishikizo: wazayuni quds hamas
captcha