IQNA

Aplikesheini mpya ya Qur'ani yazinduliwa Kuwait

22:37 - June 08, 2021
Habari ID: 3473990
TEHRAN (IQNA)- Aplikesheni mpya ya Qur'ani iliyopewa jina la 'Ayatul Ahkam' imezinduliwa hivi karibuni nchini Kuwait.

Aplikesheni hiyo imezinduliwa na Sheikh Ali Hassan Ghaloum na inajumuisha maamurisho ya kidini na masuala ya kifiqhi ambayo yametajwa katika Qurani Tukufu.

Aidha aplikesheni hiyo ina taarifa mbali mbali za Qurani kama vile ibara za Qur'ani na maneneo yanayoshabihiana na halikadhalika maelezo kuhusu aya. Aidha aplikesheni hiyo inabaini sura zilizoteremshwa Makka na Madina.

Applikesheni hiyo inaweza kupakuliwa katika  aahkam.com au  play store kwa simu za mfumo wa Android.

Kwa maelezo zaidi kuhusu utumizi wa aplikesheni hiyo unaweza kutembelea  https://youtu.be/XEJtf4o0wtQ

3976018

captcha