Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Jumatatu alizungumza kwa simu na Rais Recep Tayyep Erdogan wa Uturuki na kutoa mkono wa heri na fanaka kwa taifa na nchi rafiki na jirani ya Uturuki kwa kuwadia Sikukuu ya Idul-Fitr na kueleza kuwa: Siasa za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kukuza uhusiano wa pande zote na nchi za kanda hii hususan Uturuki.
Kwa upande wake Rais wa Uturuki Recep Tayyep Erdogan ametoa mkono wa baraka heri ya Idul-Fitr kwa taifa na serikali ya Iran na akasema kwamba, anataraji kuwa sikukuu hii italeta afya, ustawi na furaha kwa Uimwengu wote wa Kiislamu.
Rais wa Uturuki aidha ameeleza hamu yake ya kufanya ziara hapa Tehran na kuongeza kuwa: Uturuki inataka kufanya mazungumzo na kubadilishana mawazo na Iran kuhusu matukio ya kieneo na kimataifa na pia kutekeleza mipango ya kupanua ushirikiano wa pande mbili na kimataifa hasa kuzidisha kiwango cha biashara kati yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.