IQNA

Fikra za Kiislamu

Nini Maana ya Tasbih?

20:23 - October 04, 2022
Habari ID: 3475879
TEHRAN (IQNA) - Wanadamu wanamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa sifa na majina tofauti. Sifa hizi zinarejelea katika ukuu, nguvu, na huruma ya Mungu miongoni mwa sifa zingine.

Wakati huo huo, wengine wanaamini kwamba sio wanadamu tu, bali viumbe vingine pia humkumbuka Mungu.

Tasbih maana yake ni kuwa, Mwenyezi Mungu anatangaza hana sifa ambazo washirikina wanamnasibisha nazo.

Sura saba za Qur'ani Tukufu zinaanza na Tasbih, zikiwemo As-Saff, Al-Ala, Al-Hadid, Al-Jumu'ah, At-Taghabun, Al-Hashr, na Al-Isra. Neno Tasbih na  mnyambuliko wake limetumika mara 90 katika Qur'ani Tukufu huku neno "Subhan" .likiwa ndilo linalotajwa zaidi. Mengi ya maneno haya yana maana ya kumtakasa na kumtukuza Mwenyezi Mungu.

Tasbih wakati mwingine hutajwa pamoja na sifa (Hamd) kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Baadhi ya wafasiri wanaamini kwamba hii ina maana kwamba mwanadamu hawezi kusema Tasbih peke yake bali anasema hivyo kwa rehema za Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu, chochote kilichomo ndani ya ulimwengu kinamtukuza Mwenyezi Mungu: “Zinamsabihi zote mbingu saba na ardhi na vyote viliomo ndani yake. Na hapana kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake. Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye maghfira.” (Surah Al-Isra, aya ya 44)

Dhihirisho la wazi kabisa la Tasbih ni usemi "subḥāna -llāhi" [Ametakasika Mungu] kwani pia ni sehemu ya misemo inayotumiwa katika sala za kila siku: "subḥāna rabbiya l-ʿadīmi wa-bi-ḥamdih" [Ametakasika Mola wangu Mkubwa. , na kwa sifa zake] na “subḥāna rabbiya l-ʾaʿlā wa-bi-ḥamdih” [Ametakasika Mola wangu Mtukufu, na kwa sifa zake].

Tasbih hasa inarejelea maneno "subḥāna -llah" lakini kwa ufafanuzi mpana zaidi, pia inajumuisha Dhikr zingine kama vile "Allahu ʾakbar" [Mungu ni Mkuu kuliko kila kitu], "al-ḥamdu lillah" [Sifa njema zote ni za Mungu] , na "lā ʾilāha ʾillā -llah" [Hakuna mungu ila Mungu]. Maneno haya yanajumuisha Al-Tasbihat al-Arba'a ambayo inasomwa katika sala za kila siku.

Qur’ani Tukufu inawashauri waumini kusema Tasbih katika nyakati mbalimbali kwani kumekuwa na msisitizo wa kuisema wakati wa kuchomoza kwa jua na kuchwa kwa jua. “ Yavumilie haya wayasemayo. Na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumsifu kabla ya kuchomoza jua, na kabla halijachwa, na nyakati za usiku pia umtakase, na ncha za mchana ili upate ya kukuridhisha. ” (Surah Taha, aya ya 130)

captcha