IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Khazaei wa Iran ashika nafasi ya 3 katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Uturuki

20:02 - October 06, 2022
Habari ID: 3475887
TEHRAN (IQNA)- Hafla ya kufunga Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Uturuki ilifanyika Jumatano usiku katika mji mkuu wa nchi hiyo, Ankara.

Washindi wakuu katika kategoria mbili za mashindano hayo, yaani kusoma Qur'ani na kuhifadhi Qur'ani nzima, walitajwa na kutunukiwa katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki.

Katika kategoria ya qiraa au kisomo, wawakilishi wa Uturuki na Morocco walishaka nafasi ya kwanza na ya pili na huku Khazaei wa Iran akipata nafasi ya tatu

Katika kategoria ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu,, mwakilishi wa Yemen alinyakua tuzo ya juu wawakilishi wa Somalia na Syria wakishika nafasi ya pili na ya tatu mtawalia.

Hossein Khani ambaye aliiwakilisha Iran katika kategoria hii alifanikiwa kuingia katika raundi ya mwisho lakini hakuweza kuwa katika kundi la watatu bora. Khazaei na Khani watarejea Iran Jumapili asubuhi.

Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Kurugenzi ya Masuala ya Kidini ya Uturuki (Diyanet) kwa kushirikisha wanaosoma na kuhifadhi Qur'ani kutoka nchi mbalimbali.

Toleo la saba lilifanyika mnamo 2019 na hafla hiyo iliahirishwa kwa miaka miwili kwa sababu ya janga la COVID-19.

3480737

captcha