IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Qur’ani ya Kimataifa kwa Wanawake Yakamilika

20:14 - October 06, 2022
Habari ID: 3475888
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya Duru ya Sita ya Tuzo ya Kimataifa ya Qur’ani ya Sheikha Fatima Bint Mubarak kwa wanawake yalihitimishwa huko Dubai, UAE.

Kikao cha mwisho cha shindano hilo kilifanyika Jumatano jioni katika Jumuiya ya Utamaduni na Sayansi ya Dubai.

Kundi la mwisho la washindani walioonyesha vipaji vyao vya Qur'ani ni wahifadhi tisa kutoka Mauritania, Burundi, Uganda, Rwanda, Niger, Kongo, Afrika Kusini, Ghana na Gambia.

Mashindano hayo yalianza Jumamosi kwa kushirikisha wawakilishi kutoka nchi 136.

Washindi watatangazwa na kutunukiwa katika hafla ya kufunga Ijumaa, kulingana na Ibrahim Bu Milha, mshauri wa Mtawala wa Dubai kwa Masuala ya Kiutamaduni na Kibinadamu na mwenyekiti wa Tuzo ya Kimataifa ya Dubai ya Qur'ani Tukufu (DIHQA).

Alibainisha kuwa washindani ni chini ya umri wa miaka 25 na wamehifadhi Qur'an nzima huku wakiwa ni wenye ujuzi juu ya sheria za Tajweed.

Kulingana na afisa huyo, mshindi wa juu wa shindano hilo atapata zawadi ya pesa taslimu dirham 250,000 huku watakaoibuka wa pili hadi wa kumi wakipewa dirham 200,000 hadi 35,000.

DIHQA kila mwaka huandaa hafla ya kimataifa ya Qur'ani kwa wanawake kutoka nchi mbalimbali.

3480735

captcha