IQNA

Nidhamu Katika Qur'ani/ 5

Kujistahi na nidhamu ya kihisia kulingana na Qur'ani

20:54 - April 24, 2024
Habari ID: 3478728
IQNA - Sababu kuu ya hisia nyingi zisizohitajika ni ukosefu wa kujistahi au ile hisia ya kujiheshimu.

Ikiwa mtu anatambua kwamba ukuu na adhama yake ya kweli inahusiana na imani kwa MwenyeziMungu na haitokani na mambo ya nje, atakuwa salama dhidi ya hisia zisizofaa katika matukio yote.

Iwapo mwanadamu atakuwa na Imani kutokana na hadhi aliypewa na Mwenyezi Mungu, basi jambo hilo litamsaidia kupata  uwezo wa kujidhibiti na na kuzuia matukio mbalimbali na kushindwa kuwa na matokeo yenye uharibifu katika hali yake ya akili.

Qur’ani Tukufu inasema: “Wala msilegee (msife moyo), wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini.” (Aya ya 139 ya Surah Al Imran)

Huzn (huzuni) hutokea kwa mtu anapopoteza kitu au kushindwa kuwa na kitu anachopenda kuwa nacho. Maneno “msife moyo” yanawafundisha Waislamu kwamba ikiwa wana imani kwa Mwenyezi Mungu, hawapaswi basi kuruhusu azma yao kudhoofika au ikiwa wameshindwa kupata ushindi dhidi ya maadui, wasikatishwe tamaa, kwa wako katika upande wa haki.

Kwa kweli, hisia nyingi mbaya hutoka kwa ukosefu wa kujistahi. Akitambua kwamba ukuu na adhama yake ya kweli inahusiana na imani kwa Mwenyezi Mungu na haitokani na mambo ya nje, mwanadamu atakuwa salama mbele ya  hisia hasi na atakuwa mtulivi katika akikumbana na matukio yote yasiyopendeza.

Katika Aya ya 65 ya Sura Yunus, “Wala yasikuhuzunishe maneno yao. Hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua."

Qur'ani imesisitiza kuwa ushindi na uwezo wote ni wa Mwenyezi Mungu na si mwingine. Aya inamwambia Mtukufu Mtume Muhammad  (SAW) kwamba yale wanayoyasema makafiri na kukanusha kwao haki hayana athari yoyote kwa hadhi na itibari yake na, kwa hiyo, hakuna haja ya kuhuzunika.

3487998

Kishikizo: qurani tukufu
captcha