IQNA

Msomi wa Kiislamu wa Nigeria aliyepiga vita misimamo mikali afariki

21:30 - December 24, 2020
Habari ID: 3473486
TEHRAN (IQNA) -Msomi wa Kiislamu aliyeongoza mkakati dhidi ya misimamo mikali ya kidini, Sheikh Ahmed Lemu, ameaga dunia leo Alkhamisi akiwa na umri wa miaka 90.

Bintiye Sheikh Lemu, Maryam Lemu ameweka taarifa kupitia ukurasa wake wa Twitter ifuatavyo:

“Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Rajiun,ni kwa masikitiko makubwa na katika hali ya kumcha Allah tunatangaza kuaga dunia baba yetu, Dakta Jaji Sheikh Ahmed Lemu katika mji wa Minna.”

Sheikh Lemu alikuwa mwanazuoni maarufu na mtaalamu bingwa wa sheria za Kiislamu. Aidha Sheikh Lemu ambaye alikuwa Kadhi mstaafu atakumbukwa kwa kuongoza kamati iliyoundwa na rais Goodluck Jonathan wa Nigeria mwaka 2011 ili kuchunguza ghasia zilizobuka katika uchaguzi wa rais mwaka huo.

Sheikh Lemu halikadhalika alikuwa mstari wa mbele kukabiliana na changamoto za usalama na misimamo mikali ya kidini miongoni mwa Waislamu kaskaizni mwa Nigeria.

Alianzisha Taasisi ya Da’awa (Uhubiri) ya Kiislamu kwa lengo la kukabiliana na misimamo mikali ya kidini mbali na kuwa mtetezi wa haki za wanawake Waislamu.

3943143

Kishikizo: lemu nigeria waislamu
captcha