IQNA

Mvumbuzi Saudia ametayarisha Qur’ani ya kidijitali kwa lugha ya Braille

13:43 - January 31, 2021
Habari ID: 3473609
TEHRAN (IQNA) - Mvumbuzi wa Saudi Arabia ametangaza kuwa kufanikiwa kutayarisha nakala ya Qur’ani Tukufu ya kielektroniki kwa lugha ya Braille ambayo hutumiwa na watu wenye ulemavu wa macho.

Idara ya Masuala ya Haramein Sharifein nchini Saudia imetangaza kuwa  tayari kumsaidia mvumbuzi huyo kutayarisha kazi yake hiyo kwa ajili ya kutumiwa na wenye ulemavu wa macho.

Kwa mujibu wa taarifa,  mkuu wa  Idara ya Masuala ya Haramein Sharifein ametangaza kuwa amekutana na mvumbuzi huyo, Mashaal Al Harsani kwa ajili ya kujadili kuhusu Qur’ani hiyo ya kidijitali ya lugha ya Braille na namna itakavyoundwa na hatimaye kuwafikia wenye ulemavu wa macho.

Amesema lengo la kutayarishwa Qur’ani ya kidijitali kwa lugha ya Braille ni kuwahimiza wenye ulemavu wa macho kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

Alfabeti ya Braille, huwasaidia watu wasioona au wenye ulemavu wa macho kusoma. Braille husomwa na wenye ulemavu wa macho kwa kupitisha vidole juu ya karatasi.

3950942

Kishikizo: braille qurani tukufu
captcha