IQNA

Kikao cha Kusoma Qur'ani

Kikao cha Qur'ani cha Wanawake wa Ulimwengu wa Kiislamu chafanyika Tehran

14:00 - April 20, 2023
Habari ID: 3476892
TEHRAN (IQNA) – Kikao cha Kusoma Qur’ani Tukufu cha Wanawake wa Ulimwengu wa Kiilamu kinafanyika leo hapa mjini Tehran kwa kushirikisha wanawake kutoka Iran na kwingineko katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kikao hicho kinachojulikana kama  Khayrat Hisan,  kimeandaliwa  siku ya 29 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na kabla ya Eid al-Fitr.

Ukumbi wa Vahdat katika mji mkuu Tehran utakuwa mwenyeji wa kikao hicho cha  Qur'ani.

Makumi ya wanawake wanaharakati wa Qur'ani wakiwemo wahifadhi, wasomaji na maafisa wa taasisi za Qur'ani kutoka Iran, Iraq, Syria, Indonesia na nchi nyingine watashiriki katika hafla hiyo ya Qur'ani.

Kikao hicho kinajumuisha usomaji wa Qur'ani na qasida.

Muslim World Women’s Quranic Circle Planned in Tehran

Baada ya kukamilika Ramadhani, sherehe za Idul Fitra zinatazamiwa kuwa katika Ijumaa au Jumamosi kwa kuzingatia muandamo wa mwezi mpevu wa mwezi wa Shawwal. Ramadhani ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu na ni mwezi wa Saumu ya kujizuia kula na kunywa kuanzia Alfajiri hadi Magharibi. Ni kipindi cha sala, saumu, utoaji wa sadaka na ukitirishaji wa usomaji Qur'ani Tukufu.

4135395

captcha