IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Mwanazuoni wa Kiislamu: Kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu kumechafua taswira ya Uswidi

19:03 - July 30, 2023
Habari ID: 3477360
STOCKHOLM (IQNA) - Mwanazuoni wa Kiislamu mwenye makazi yake nchini Uswidi anasema vitendo vya mara kwa mara vya kuvunjiwa heshima Qur'ani katika nchi hiyo ya eneo la Nordic barani Ulaya vinaiweka sura ya Uswidi hatarini.

Sheikh Yusuf Qarut, mwakilishi wa Baraza Kuu la Kishia la Kiislamu la Lebanon nchini Uswidi, aliyasema hayo katika ujumbe wa video uliorekodiwa awali kwa ajili ya kongamano la kimataifa ambalo limejadili kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu kwa mtazamo wa haki za binadamu.

Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani (IQNA) limeandaa mkutano huo kwa njia ya intaneti, uliopewa jina la " anuani ya:  "Kuangazia Kuvunjiwa Heshima Qur'ani Tukufu kwa Mtazamo wa Kimataifa wa Haki za Kibinadamu," siku ya Jumapili.

"Taswira ya Uswidi kama nchi iliyoendelea ambayo ilikuwa mfano wa kuigwa kwa ubinadamu na kuishi pamoja kati ya makundi mbalimbali iko hatarini," alisema mwanazuoni huyo.

Alibainisha kuwa matukio ya hivi majuzi yanatishia "amani na maelewano ya ndani" nchini Uswidi pamoja na uhusiano wake wa nje.

Matamshi hayo yanakuja wakati mkimbizi wa Iraq mwenye makazi yake Uswidi ameidharau Qur'ani Tukufu mara nyingi katika kipindi cha miezi miwili iliyopita baada ya mamlaka ya Uswidi kuruhusu matukio hayo kutokea kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.

Vitendo hivyo vya kukufuru vimelaaniwa vikali na mataifa ya Kiislamu na yasiyo ya Kiislamu kutoka kote duniani na Stockholm imehimizwa kuangalia upya sheria zake na kuzuia vitendo vingine vya uchochezi.

“Uhuru wa kusema na uhuru wa mawazo ni baadhi ya dhana bora na za hali ya juu zaidi za binadamu, lakini watu hawa wanachukua fursa ya tafsiri isiyo wazi ya nadharia hii, na ndiyo maana tunaendelea kuwaambia kwamba waifafanue ili isiwe chombo cha mambo ya kizushi,” Qarut alisema.

Kulingana na mtaalam huyo, ni watu wa Uswidi ambao hupata hasara kutokana vitendo hivi vya itikadi kali.

"Historia yetu ya Kiislamu imejaa nyakati ambapo watawala dhalimu walijaribu kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa maneno yao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyeiteremsha hii Qur'ani Tukufu na Yeye ndiye anayeisimamia," alibainisha, akiashiria aya ya 9. ya Surah al-Hijr isemayo: “Tumeiteremsha Qur’an na Sisi ni Walinzi wake."

3484561

Habari zinazohusiana
captcha