IQNA

Utamaduni wa Qur'ani

Mtaalamu wa Kipindi cha Televisheni cha Mahfel: Mwenyezi Mungu Hubariki Kazi za Qur’ani­­

22:10 - March 18, 2024
Habari ID: 3478537
IQNA – Kipindi maalum cha televisheni cha Mwezi wa Ramadhani  cha ‘Mahfel’ ni kazi ya Qur’ani na ndiyo maana kimebarikiwa na Mwenyezi Mungu, mmoja wa wataalamu wa kipindi hicho alisema.

Hujjatul Islam Gholam Reza Ghasemiyan alizungumza na IQNA kuhusu programu hiyo maarufu na nafasi yake ndani yake.

Onyesho la msimu wa pili wa kipindi cha TV lilianza kwenye Kanali ya 3 ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani Jumanne.

Hutangazwa kabla magharibi kila siku katika mwezi mtakatifu wa Ramadhani, na hivyo ni fursa nzuri ya kiroho kwa watazamaji wanapojitayarisha kufuturu.

Kwa kujikita katika Qur'ani Tukufu, kipindi hiki kinalenga kuimarisha muda mfupi uliosalia kabla ya kufuturu waliofunga kuangazia mijadala yenye mafunzo na usomaji Qur’ani wenye kuvutia.

Hujjatul Islam Ghasemiyan amesema pamoja na kwamba kulikuwa na wasiwasi kwamba msimu wa pili hautafanikiwa kama ule wa kwanza lakini kuna suala muhimu linalofanyika na hapo ndipo jambo linapofanywa kwa ajili ya Qur'ani hupata baraka za Mwenyezi Mungu.

Alisema ilisemekana kabla ya kipindi hiki kwamba jumbe za Qur'ani zinapaswa kuwasilishwa ndani ya masomo mengine na sio moja kwa moja, lakini kufaulu kwa Mahfel kulionyesha kuwa njia hii iliyotumika ni sahihi.

Msomi huyo alibainisha kuwa anachofanya katika kipindi hiki ni kufasiri aya za Qur’an kwa njia sahali na yenye mvuto.

Alisema baada ya kuona mafanikio ya Mahfel, aliacha shughuli nyingine nyingi na amejitolea kufanya kazi za Qur'ani pekee.

Alipoulizwa kuhusu wataalamu wanaohudumu katika kipindi hicho, Hujjatul Islam Ghasemiyan amesema wao ni miongoni mwa waliobobea katika fani yao, akiwemo Hamed Shakernejad ambaye ni mmoja wa maqari wakubwa duniani, Sayyid Hassanayn al-Hulw ambaye ni qari maarufu wa Haram Takatifu ya Hadhrat Abbas (AS), Ahmad Abolqassemi ambaye ni mwalimu mashuhuri wa Qur'ani nchini Iran, na Rizwan Darwish kutoka Syria.

3487644

captcha