IQNA

Wakimbizi Waislamu Warohingya wahamishiwa kisiwa kipya

15:22 - January 06, 2021
Habari ID: 3473530
TEHRAN (IQNA) –Bangladesh imewahamisha Waislamu 1,804 wakimbizi wa jamii ya Rohiingya kutoka katika kambi ya wakimbizi ya Cox's Bazar na kuwapeleka katika kisiwa cha mbali ambacho hadi sasa hakikuwa na wanadamu katika Ghuba ya Bengali .

Mashirika ya haki za binaadamu yamelalamikia vikali kitendo hicho cha serikali ya Bangladesh na kusema usalama wa wakimbizi hao uko hatarini.

Itakumbukwa kuwa wimbi jipya la mauaji, mashambulizi na ubakaji wa jeshi la Myanmar katika mkoa wa Rakhine kuwalenga Waislamu wa Rohingya, lilianza tarehe 25 Agosti mwaka 2017 ambapo zaidi ya Waislamu elfu sita waliuawa na wengine elfu nane kujeruhiwa. Aidha zaidi ya Waislamu wengine milioni moja wa jamii hiyo walilazimika kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh huku wengine wakipata hifadhi katika nchi kama vile India, Thailand na Malaysia.

Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein aliesema kuwa uhalifu unaofanywa na Mabudha kwa himaya ya serikali nchini Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya ni mauaji ya kimbari.

 

3473614

captcha