IQNA

Adhana yapigwa marufuku katika jela za Israel

12:50 - February 19, 2014
Habari ID: 1377228
Kundi la kutetea haki za binadamu la Palestina limetangaza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umepiga marufuku adhana katika jela zake wanakoshikiliwa maelfu ya Waislamu wa Kipalestina.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari za Qur’ani la Kimataifa (IQNA) kutoka kwa taasisi ya Palestiine-info, maafisa wa jela za eneo la Patakh Kiva wamepiga marufuku kutoa adhana katika jela za eneo hilo.
Hatua hiyo imewachukiza sana mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela hizo. Habari zinasema kuwa maafisa wasimamizi wa jela hizo wamewatishia mateka wa Kipalestina katika korokoro za Israel kwamba iwapo watatoa adhana watafungwa miguu na mikono yao katika nyakati za usiki.
Jumuiya za kutetea haki za binadamu huko Palestina zimeitaka jamii ya kimataifa kushughulikia dhulma wanazokabiliana nazo Wapalestina hususan mateka wa Kipalestina katika korokoro za Israel na kuchukua hatua za kukomesha ukatili huo haraka iwezekanavyo.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa hivi karibuni pia Naibu Meya wa mji wa Haifa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu alipiga marufuku adhana inayotolewa nyakati za ibada ya Swala katika eneo hilo, suala ambalo limepingwa vikali na Wapalestina.

1376688

Kishikizo: adhana palestina israel
captcha