IQNA – Bi Zubaydah Taysert, Waziri wa Utamaduni wa Thailand, alifanya ziara rasmi katika Makumbusho ya Urithi wa Kiislamu na Kituo cha Elimu ya Qur'ani kilichoko katika wilaya ya Yingluck, Jumamosi tarehe 18 Oktoba 2025, kabla ya uzinduzi rasmi wa majengo hayo.
IQNA-Sheikh Mamosta Fayeq Rostami, msomi maarufu wa Ahul Sunna na mwakilishi wa watu wa Kurdistan katika Baraza la wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Iran amesisitiza kuwa Qurani Tukufu si tu kitabu cha ibada, bali ni waraka kamili unaoelekeza maisha ya binadamu katika nyanja za uchumi, utamaduni na siasa
IQNA-Awamu ya mwisho ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya 48 imezinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika asubuhi ya Jumamosi katika mji wa Sanandaj, mkoa wa Kurdistan.
IQNA-Bunge la Ureno limeidhinisha muswada unaopendekeza marufuku ya uvaaji wa Hijabu aina ya Niqabu au Burqa kwa sababu za kijinsia au za kidini katika maeneo mengi ya umma. Muswada huo uliwasilishwa na chama cha mrengo wa kulia kinachoitwa Chega, na unalenga hasa burqa na niqab zinazovaliwa na wanawake Waislamu.
IQNA-Katika mji wa Mason, jimbo la Ohio nchini Marekani, kuna shule inayojulikana kama ICM Learning Academy ambayo hufundisha wanafunzi si tu kusoma Qur’ani Tukufu bali pia kuifahamu na kuikumbuka kwa moyo wote.
IQNA-Katika Aya ya pili ya Surah Al-Ma’idah, Mwenyezi Mungu Mtukufu ametaja amri nane muhimu, ambazo ni miongoni mwa maagizo ya mwisho aliyoteremshiwa Mtume Muhammad (Rehema na Amani zimshukie). Miongoni mwa amri hizo ni kushikamana kwa pamoja katika njia ya wema na uchamungu.
Mtume Mtukufu Muhammad (SAW) amesema:
“Kwa hakika mja hupata daraja ya aliyefunga na anayesimama (kwa ibada usiku) kwa sababu ya tabia njema.”
(Bihar al-Anwar, Jildi ya 68, Ukurasa wa 386)
IQNA-Itamar Ben Gvir, Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni, licha ya onyo kutoka kwa Waqfu wa Kiislamu, ameuvamia tena Msikiti wa Al-Aqsa jijini Quds (Jerusalem) kwa mara ya pili ndani ya wiki moja.
IQNA-Hafla ya kuvienzi vyuo vikuu vilivyofanya vyema pamoja na kamati ya majaji walioshiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya vyuo vikuu, yaliyopewa jina la "Al-Nur", imefanyika katika Chuo Kikuu cha Al-Ameed nchini Iraq.
IQNA – Toleo la pili la Mashindano ya Kimataifa ya Usomaji na Kuhifadhi Qur’ani Tukufu nchini Kazakhstan limehitimishwa kwa hafla rasmi iliyofanyika mjini Astana.
IQNA-Wizara ya Wakfu wa Kidini ya Misri imemteua rasmi Qari Dkt. Ahmed Ahmed Nuaina kuwa Sheikh al-Qurra, yaani Kiongozi Mkuu wa Wasomaji wa Qur'anI nchini humo.
IQNA – Katika juhudi za kuboresha huduma kwa mahujaji na wakazi wa Makkah, kampuni ya RUA Al Haram Al Makki imetangaza mradi mkubwa wa maendeleo unaojulikana kama Lango la Mfalme Salman , utakaojengwa karibu na Msikiti Mkuu wa Makkah. Mradi huu utaongoza takriban maeneo 900,000 ya kuswali ndani na nje ya jengo.
IQNA – Chuo Kikuu cha Al-Ameed kimeandaa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'an yanayojulikana kama “Qur'an Al-Nur”, yakihusisha wanafunzi kutoka zaidi ya vyuo vikuu 60 vya ndani na nje ya Iraq.