IQNA

Bunge la Ulaya kufuta kinga ya Le Pen

11:54 - June 23, 2013
Habari ID: 2551056
Kamati ya Sheria ya Bunge la Ulaya imeunga mkono suala la kufutwa kinga ya kisheria ya kiongozi wa chama cha Harakati ya Kitaifa cha Ufaransa (Front National (FN)) Marine Le Pen kwa sababu ya kuwadunisha Waislamu.
Kamati ya Sheria ya Bunge la Ulaya ambayo ilikuwa ikijibu ombi la viongozi wa Ufaransa la kufutwa kinga ya kisheria ya Marine Le Pen imetangaza kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwamba kinga hiyo ya kutofikishwa mahakamani itaondolewa kwa mwanasiasa huyo mbaguzi.
Mwaka 2012 Wizara ya Sheria ya Ufaransa ilimtaka Spika wa Bunge la Umoja wa Ulaya kufuta kinga ya kufikishwa mahakamani kiongozi wa chama cha Front National (FN). Iwapo kinga hiyo itaondolewa mbunge huyo mbaguzi wa Umoja wa Ulaya atafikishwa mahakamani nchini Ufaransa kwa kuwashabihisha Waislamu waliokuwa wakisali na wavamizi wa kinazi.
Katika hotuba aliyotoa mwaka 2010 katika mji wa Lyon, Le Pen aliwafananisha Waislamu waliokuwa wakitekeleza ibada ya Swala katika mitaa ya nchi hiyo kuwa ni sawa na wavamizi wa kipindi cha manazi. 1246288
captcha