IQNA

Utawala wa Israel waendelea kuwakandamiza Wapalestina

22:16 - October 28, 2015
Habari ID: 3407233
Wanajeshi wa utawala katili wa Kizayuni wanaendelea kufanya jinai katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu kama vile Ukingo wa Magharibi na Ukanda Ghaza.

Idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi tangu ilipoanza Intifadha mpya ya taifa hilo madhlumu imefikia watu 64, baada ya kijana mwengine wa Kipalestina kupigwa risasi na kuuliwa shahidi na Wazayuni. Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, jana usiku wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walimpiga risasi na kumuua shahidi kijana mmoja wa Kipalestina katika mji wa al Khalil, kusini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Mapema hiyo jana pia, wanajeshi katili wa Israel waliwashambulia Wapalestina waliokuwa wanaandamana katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan baada ya kushiriki kwenye maziko ya kijana mmoja mwenye umri 19 wa Kipalestina aliyeuliwa shahidi na Wazayuni siku ya Jumatu. Wapalestina hao walioshiriki kwenye maziko hayo ya Eyad Jaradat walishambuliwa kwa risasi hai na mabomu ya kutoa machozi na Wazayuni katika mji wa al Akhalil. Makundi ya Kipalestina yameitisha "maandamano ya hasira" katika mji mzima wa al Khalil ili kuonesha uungaji mkono wao kwa familia za wahanga wanaouliwa na wanaejshi wa utawala wa Kizayuni kwa madai ya kujaribu kuwashambulia walowezi wa Kizayuni.

3402878

captcha