IQNA

Saudia yapiga marufuku adhana katika misikiti ya Mashia

12:42 - April 01, 2016
Habari ID: 3470222
Viongozi wa utawala wa Aal Saud nchini Saudi Arabia wamepiga marufuku kutangazwa adhana katika misikiti ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mkoa wa Al-Hasa, mashariki mwa nchi hiyo.

Viongozi wa utawala wa Riyadh wametoa dikrii kadhaa ambazo utekezaji wake umeanza rasmi leo kwa lengo la kuzuia kutangazwa adhana katika misikiti ya Mashia.

Viongozi wa utawala wa Aal Saud wametoa amri pia ya kufupishwa hotuba za Sala ya Ijumaa katika misikiti ya eneo la al-Hafuf na kutaka misikiti isiendelee kuwa wazi zaidi ya saa sita na nusu mchana.

Katika kuendeleza sera zake za kuwakandamiza Waislamu wa madhehebu ya Shia, utawala wa Aal Saud hapo kabla ulimtia nguvuni Ayatullah Hussein al-Radhi, Imamu wa Ijumaa wa mkoa wa Al-Hasa kwa tuhuma za kuukosoa utawala huo.

Tangu lilipoanza vuguvugu la Mwamko wa Kiislamu mwaka 2011 katika nchi za Kiarabu za eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika, nchi nyingi za Kiarabu za eneo hili ikiwemo Saudi Arabia zimekuwa uwanja wa maandamano ya wananchi ya kupinga tawala za nchi hizo.

Nchini Saudia wimbi la maandamano ya upinzani limekuwa likishuhudiwa zaidi katika maeneo ya Waislamu wa Kishia mashariki mwa nchi hiyo. Utawala wa Aal-Saud umetumia mkono wa chuma kuzima maandamano hayo ya wananchi ambapo hadi sasa mamia ya watu wameuliwa au kutiwa gerezani.

3459416

captcha