Kuhusiana na suala hili, Idara ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala
ya Palestina OCHA siku ya Ijumaa ilitoa taarifa na kukosoa vikali kuenea
jinai za Israel dhidi ya Wapalestina na kubaini kuwa katika kipindi cha
wiki moja iliyopita, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamewaua shahidi
Wapalestina kadhaa na kuwajeruhi wengine 85. Aidha katika kipindi cha
wiki moja sasa wanajeshi wa Israel wamehujumu na kubomoa makumu ya nyuma
za Wapalestina.
Kwa mujibu wa ripoti ya OCHA, kwa kisingizio cha kutafuta njia za chini
ya ardhi zinazotumiwa na Hamas katika eneo la mapaka wa Ghaza na Misri,
katika kipindi cha siku nne zilizopita, jeshi la Israel limetekeleza
mashambulizi makubwa katika eneo hilo. Siku ya Ijumaa eneo la Khan Yunis
mashariki mwa Ghaza lilishuhudia mashambulizi ya kuogofya ya Utawala wa
Kizayuni ambalo Wapalestina kadhaa waliuawa shahidi au kujeruhiwa.
Matukio ya wiki moja iliyopita Palestina yanaashiria kushadidi
ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni na kueneza sera za kujitanua za
utawala huo.
Ni kwazi kuwa, kwa jinai zake hizo, utawala wa Kizayuni unatafuta fursa
ya kueneza sera zake za kujitanua, uporoaji ardhi, na kuwakamdamiza
wapigania ukombozi wa Palestina. Utawala huo unatumia nguvu za kijeshi
kufikia malengo yake haramu.
Kuedelea ukandamizaji na ukatili wa utawala wa Kizayuni dhidi ya watui
waiso na ulinzi wa Palestina ni ukiukwaji wa wazi wa mikataba ya
kimataifa ya Geneva. Hivi sasa walimwengu wanafahamu jinai dhidi ya
binadamu za utawala wa Kizayuni na suala ambalo imepelekea kuwepo
malalamiko dhidi ya utawala huo dhalimu wa Israel.
Hii ni katika hali ambayo ripoti za kimataifa dhidi ya Israel
hazifuatiliwi katika Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa kutokana na
vizingiti vinavyowekwa na Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi katika
baraza. Himaya hiyo ya Marekani imepelekea utawala wa Kizayuni upate
kiburi zaidi kutekeleza jinai zake.
Pamoja na kushahidi jinai za utawala wa Kizayuni kumepelekea hali ya
Wapalestina kuwa mbaya, lakini ukandamizaji huo haujawafanya Wapalestina
wasalimu amri mbele na utawala wa Kizayuni.
Watu wa Palestina kwa kutegemea mapambano yao dhidi ya Uzayuni,
wamesisitiza kuendelea kusimama kidete mbele ya utawala wa Kizayuni na
kupelekea utawala huo kufeli katika njama zake, na hata wakuu wa Israel
wamekiri hilo.
Kuhusiana na maudhui hii, mkaguzi mkuu wa Utawala wa Kizayuni amekosoa
utendaji kazi wa waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu katika
hujuma yake ya siku 50 dhidi ya ukanda wa Ghaza mwezi Juni mwaka 2014.
Yosef Shapira Mkaguzi Mkuu wa Israel katika ripoti yake kuhusu utendaji
kazi wa baraza la mawaziri la Israel katika vita hivyo vya siku 50
dhidi ya ghaza amesema, "utendaji wa Netanhayu katika vita hivyo ulikuwa
dhaifu na vita hivyo vilimalizika wka hasara ya Israel."
Kanali ya pili ya televisheni ya utawala wa Kizayuni imesema ripoti hiyo
kuhusu vita vya siku 50 vya Ghaza ni bomu katika siasa za utawala huo
na kwamba ripoti hiyo ikitangazwa hadaharani basi kutaibuka mgogoro
mkubwa.
Utawala wa Kizayuni unaendeleza hujuma zake dhidi ya Ghaza katika hali
ambayo hujuma hizo si tu kuwa hazijafikia malengo yaliyoainishwa bali
pia zimepelekea kufeli zaidi utawala huo ghasibu na hivyo kupelekea
kuiubuka mifarakano zaidi ndani ya utawala huo.
Katika hali kama hii, utawala wa Kizayuni umeanzisha duru mpya ya hujuma
dhidi ya ukanda wa Ghaza ili kujaribu kufunika kufeli kwale na pia
kupotosha fikra za umma ndani ya utawala huo.
Lakini matukio ya Palestina yanaashiria kuwa chokochoko mpya za utawala
wa Kizayuni Ghaza hazitakuwa na natija nyingine ghairi ya kutumbukia
utawala huo katika kinamasi cha kujitakia wenyewe.
3459732