Akitoa tangazo hilo, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Kuchapisha Qur'ani na Sunnah Kuwait Fahd al-Daihani amesema mradi huo utatekelezwa kwa ushirikiano na Wizara ya Masuala ya Kijamii na Leba nchini humo.
Aidha amesema bajeti kwa ajili ya mradi huo itakabidhiwa Wizara ya Biashara, Baraza la Mawaziri na Bunge kwa ajili ya kuidhibishwa.
Bajeshi ya kituo hicho imekadiriwa kuwa ni Dinari za Kuwait Milioni 12 na kinatazamiwa kuwa na uwezo wa kuchapisha nakala milioni tano za Qur'ani kwa mwaka.