Kwa mujibu wa taarifa, nchini Ujerumani sauti ya adhana kupitia vipaza sauti ilisikika katika misikiti inayosimamiwa na Jumuiya ya Waislamu wa Uturuki (DITIB) na Jumuiya ya Kitaifa ya Kiislamu (IGMG). Fahrettin Alptekin mwakilishi wa DITIB katika eneo la Essen, Ujerumani amesema kwa kawaida adhana kupitia vipaza sauti hairuhusiwi nchini Ujerumani isipokuwa tu katika nyakati maalumu.
Nchini Uholanzi adhana pia ilisikika katika vipaza sauti vya misikiti ya nchi hiyo ikiwa ni katika mkakati wa mshikamano wa watu wote katika vita dhidi ya corona. Nchini Uholanzi pia kwa kawaida adhana hairuhusiwi kupitia vipaza sauti.
Ujerumani ni nchi ya tatu kwa idadi ya watu walioambukizwa corona barani Ulaya. Hadi kufikia leo, watu 92,150 wameambukizwa corona nchini Ujerumani huku wengine 1,330 wakifariki dunia.
3471040