IQNA

Wafuasi wa dini mbali mbali waadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran

10:37 - February 13, 2021
Habari ID: 3473646
TEHRAN (IQNA) – Wafuasi wa dini mbali mbali nchini Iran siku chache zilizopita walijumuika katika maeneo yao ya ibada kuadhimisha mwaka wa 42 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Sherehe hizo ziliandaliwa kwa ushirikiano wa Idara ya Masuala ya Utamaduni na Jamii katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Ofisi ya Rais na Kituo cha Utamaduni cha Andisheh.

Mwaka huu, 22 Bahman kwa mwaka wa Hijria Shamsia sawa na Februari 10 kumefanyika sherehe kote Iran kwa mnasaba wa kutimia miaka 42 tangu Mapinduzi ya Kiislamu yalipopata ushindi kamili na kuuondoa madarakani utawala wa kifalme na kibaraka nchini Iran. Mapinduzi hayo yaliongozwa na Imam Ruhullah Khomeini , Mwenyezi Mungu Amrehemu, ambaye ni muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

 
 
captcha