IQNA

Darsa ya kuhifadhi Qur'ani inafanyika kwa njia ya intaneti Algeria

12:29 - July 08, 2021
Habari ID: 3474081
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Masuala ya Kidini Algeria imeandaa darsa maalumu ya kuhifadhi Qur'ani kwa njia ya intaneti.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Algeria, darsa hizo zinafanyika katika tovuti ya wizara hiyo iliyopewa jina la 'Maqraa' na washiriki wanapata darsa za Tajwid na kuhifadhi Qur'ani.

Wizara ya Masuala ya Kidini Algeria inasema darsa hizo ni kati ya harakati za Qur'ani zilizopangwa nchini humo wakati wa likizo ya msimu wa joto.

Washiriki katika darsa hizo wanahimizwa kuhifadhi 'Hizb' moja ya Qur'ani kila siku na pia wanajifunza misingi muhimu ya qiraa.

Wizara ya Masuala ya Kidini Algeria inasema lengo la darsa hizo ni kuimarisha ujuzi wa Qur'ani na pia kutambua vipawa kwa ajili ya mashindano ya kitaifa na kimataifa.

3982486

captcha