IQNA

Algeria yawazawadia Wapalestina Kombe la FIFA Arab Cup 2021

19:02 - December 19, 2021
Habari ID: 3474695
TEHRAN (IQNA)- Timu ya Taifa ya kandanda ya Algeria imeibuka mshindi katika mashindano ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Waarabu (FIFA Arab Cup 2021) yaliyofanyika nchini Qatar na kuwatunuku Wapalestina kombe hilo.

Kocha wa Timu ya Taifa ya Soka la Algeria, Majid Bougherra amesema kuwa timu yake inalitunuku Taifa la Palestina na watu wa Ukanda wa Gaza kombe hilo la kwanza la mataifa ya Kiarabu.

Katika kipindi chote cha mechi hiyo ya fainali iliyozikutanisha pamoja timu za taifa za Algeria na Tunisia, mashabiki wa pande mbili walikuwa wakiimba na kutoa nara za kuunga mkono mapambano ya ukombozi ya watu wa Palestina dhidi ya utawala haramu wa Israel. Vilevile bendera ya Palestina ilionekana ikipepea sambamba na bendera za Tunisia na Algeria katika uwanja wa al Bayt utakaoshuhudia ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Dunia 2022 yatafanyika nchini Qatar kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 18. 

Siku chache zilizopita Rais wa Algeria alisisitiza udharura wa nchi za Kiarabu kushirikiana kwa ajili ya kusaidia mapambano ya ukombozi ya wananchi wa Palestina dhidi ya utawala vamizi na ghasibu wa Israel.

Abdelmadjid Tebboune aliyasema hayo katika mazungumzo yake na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas aliyekuwa safari nchini Algeria ambako alitangaza msaada wa Algiers wa dola milioni mia moja kwa taifa la Palestina. 

Katika miezi ya hivi karibuni Algeria imekuwa mstari wa mbele kupinga sera na siasa za utawala ghasibu wa Israel na ukandaizaji wake dhidi ya wananchi wa Palestina.

Misimamo hiyo ya Algeria imeshuhudiwa zaidi baada ya jirani yake, Morocco, kutia saini makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel na hivi karibunivilevile kutia saini hatia ya kuanzisha ushirikiano wa kijeshi na utawala huo ghasibu.

5378828

Kishikizo: algeria palestina
captcha