Vyanzo vya habari vilisema kuwa watoto na wazee walikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa wakati waliposhambuliwa na Wazayuni wakiwa sokoni katika jiji la kalela al Quds.
Mmiliki wa duka Sami Salhab alisema kuwa mashambulizi kama hayo hutokea chini ya ulinzi wa majeshi ya Israel karibu kila siku.
Alisema walowezi hao walivamia soko hilo na kuvamia kundi la wafanyakazi walipokuwa wakifanya matengenezo katika moja ya maduka hayo.
Walowezi hao wa Kizayuni watenda jinai waliwapulizia gesi ya pilipili Wapalestina katika soko hilo, wakiwemo watoto.
Wakati huo huo, Wayahudi 255 wa Israel wenye itikadi kali walivamia Msikiti wa Al-Aqsa hapo jana na kufanya ibada za kichochezi za Talmud.
Mashambulio ya walowezi na uvamizi wa Al-Aqsa yanatarajiwa kuongezeka katika siku zijazo huku Wayahudi wakisherehekea Rosh Hashanah - Mwaka Mpya wa Kiyahudi - na Yom Kippur.