IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Mashindano ya Qur'ani Tukufu yafanyika mji mkuu wa Gambia

21:19 - January 11, 2023
Habari ID: 3476387
TEHRAN (IQNA) – Banjul, mji mkuu wa Gambia, umekuwa mwenyeji wa mashindano ya Qur'ani Tukufu yaliyojumuisha kuhifadhi, kusoma Tajweed na Tarteel.

Tawi la Gambia la Wakfu wa Mfalme  Mohammed VI wa Ulamaa wa Kiafrika liliandaa mashindano hayo.

Wasomaji 50 wa Qur'ani Tukufu kutoka sehemu mbalimbali za Gambia walishiriki katika hafla hiyo ya Qur'ani wakiwemo wanawake kumi.

Washindi wa juu walifuzu kwa mashindano ya 4 ya Afrika ya  Qur'ani Tukufu, yatakayofanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Washindi hao ni pamoja na Saad Muhammad Othman Jalu, Muhammad Ma’mun Ayub, na Abdul Bari Ahmed Dabwi.

Sheriff Abba Sanyang, Waziri wa Gambia wa masuala ya kidini, katika hotuba yake wakati wa hafla hiyo ya Qur'ani Tukufu alipongeza taasisi na serikali ya Morocco kwa juhudi zao za kukuza shughuli za Qur'ani.

Wakfu wa Mohammed VI wa Ulamaa wa Kiafrika, kwa mujibu wa waanzilishi wake, ni taasisi ya kidini ya Kiislamu inayotaka kuzuia itikadi kali za kidini na kupiga vita malumbano ya kimadhehebu baina ya Waislamu.

4113628

captcha