IQNA

Hali ya Waislamu Saudia

Vizuizi vyawekwa katika matumizi ya vipaza sauti misikitini nchini Saudi Arabia

19:14 - January 20, 2023
Habari ID: 3476436
TEHRAN (IQNA) – Matumizi ya vipaza sauti katika misikiti kote Saudi Arabia yatawekewa vikwazo, kulingana na Wizara ya Masuala ya Kiislamu, Wito na Mwongozo.

Waziri wa Masuala ya Kiislamu, Wito na Mwongozo Abdul Latif Bin Abdulaziz Al-Sheikh ameweka idadi ya vipaza sauti vya nje vinavyotumika misikitini wakati wa Adhana kuwa vinne.

Al-Sheikh ameagiza kuvitoa vipaza sauti vya nje vinavyozidi vinne kwenye misikiti yote na kuvihifadhi vya ziada kwenye ghala kwa matumizi ya baadae au kusambaza kwenye misikiti ambayo haina idadi ya kutosha.

Mwaka jana pia waziri huyo alitangaza kuweka vizuizi katika utumizi wa vipaza sauti misikitini nchini humo ambapo aliamuru misikiti yote katika ufalme huo kutumia vipaza sauti wakati wa adhana na iqama tu na pia sauti  inapaswa kuwa kiwango cha chini zaidi iliyvyo hivi sasa.

Amri hiyo ilitolewa kwa mujibu wa fatwa za wanazuoni maarufu wanaofuatwa Saudia Sheikh Mohammed bin Saleh Al Othaimeen and Saleh Al Fawzan ambao wanasema vipaza sauti vinapaswa kutumika tu wakati wa adhana na iqama.

Uamuzi huo wa kubana adhana misikitini Saudia unaonekana kuenda sambamba na mabadiliko ambayo yanaletwa na Mrithi wa Kiti cha Ufalme Mohammad bin Salman, ambaye anatakwa kuwa kiongozi asiye rasmi wa nchi. Bin Salman anatakaleza sera za kupunguza utambulisho wa kidini katika ufalme huo ambao kwa miongo kadhaa umekuwa ukitekeleza mafundisho ya pote la Kiwahhabi. Wahubiri wanaopinga sera hizo za Bin Salman wanakamatwa na kufungwa jela.

3482133

captcha