IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Ufaransa yawazuia wachezaji soka Waislamu kufuturu wakati wa mechi

15:48 - April 01, 2023
Habari ID: 3476794
TEHRAN (IQNA) – Marefa nchini Ufaransa wameamuriwa na shirikisho la soka la nchi hiyo kutositisha mechi ili kuwaruhusu wachezaji Waislamu kufuturu katika mwezi wa Ramadhani.

Tofauti na Ligi Kuu ya Uingereza ambayo inaruhusu mechi kusitishwa kwa muda ili kuwaruhusu wachezaji kabumbu wanaofunga Ramadhani kufuturu,  Shirikisho la Soka la Ufaransa limekataa kuruhusi jambo hilo.

Shirikisho hilo katika barua pepe iliyotumwa kwa waamuzi Alhamisi limesema limebaini kuwa, katika kipindi cha wiki moja mechi zimekuwa zikisimamishwa kwa muda ili kuwaruhusi wachezaji Waislamu wafuturu na kwamba hakuna ruhusa tena kufanya hivyo.

Eric Borghini, mkuu wa tume ya shirikisho ya waamuzi katika shirikisho hilo amedai kuwa hatua waliyochukua inalenga kuhakikisha kuwa masuala ya dini hayaingizwe katika kabumbu.

Wakati huohuo, wachezaji Waislamu katika timu ya taifa ya soka ya Ufaransa walishurutishwa kuahirisha mfungo wao kwa siku chache katika Mwezi wa Ramadhani.

Ramadhani ilianza Machi 23 na inatazamiwa kuendekea kwa siku 29 au 30.

Mnamo Machi 24, Ufaransa iliilaza Uholanzi 4-0 katika mechi ya kwanza ya kufuzu kwa Kundi B la EURO 2024 Uwanja wa Stade de France. Siku chache baadaye, Les Bleus walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Ireland na kuongoza Kundi B.

Kumekuwa na wachezaji kadhaa Waislamu katika kikosi cha timu ya kitaifa ya soka ya Ufaransa (Les Bleus) kwa miaka kadhaa, kama vile Zinedine Zidane, Franck Ribery, Nicolas Anelka, Paul Pogba, Ousmane Dembele, na N'Golo Kante.

Lakini kiungo wa Monaco Youssouf Fofana, na mlinzi wa Liverpool Ibrahima Konate, wachezaji Waislamu katika timu ya Ufaransa, walichaguliwa na Didier Deschamps kwa mechi za kufuzu EURO 2024 zilizoanza wiki iliyopita.

Wote wawili walicheza dhidi ya Uholanzi. Konate alikuwa kwenye kikosi cha kwanza cha 11 kwa mechi ya Ireland, lakini Fofana alikuwa miongoni mwa wachezaji wa akiba na hakucheza huko Dublin.

Katika miaka ya karibuni wimbi la chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa limeshadidi ambapo hasa katika uongozi wa Emmanuel Macron ambapo Waislamu wengi wamekuwa waiandamwa kwa mashinikizo na vitendo vya bughuda na mauadhi na hata wakati mwingine matukufu ya dini yao kutusiwa na kuvunjiwa heshima.

Ufaransa ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016, kuna zaidi ya Waislamu milioni 5.7 Ufaransa ambao ni takribani asilimia 8.8 ya watu wote nchini humo.

3483008

Kishikizo: ufaransa waislamu macron
captcha