IQNA

Qari kijana wa Algeria akisoma aya katika Surah An-Nur (+Video)

TEHRAN (IQNA) – Abdul Aziz Sahim ni qari kijana na mwenye kipaji ambaye amepata kutambuliwa nchini Algeria.

Hivi karibuni alisoma aya za Qur'ani Tukufu wakati wa sherehe za ufunguzi wa mashindano ya Taj al-Quran katika nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika.

Katika onyesho lake katika hafla hiyo iliyofanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, alisoma aya ya 35 ya Surah An-Nur:

 

 

 

 

 

 Mwenyezi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi. Mfano wa Nuru yake ni kama shubaka lenye kuwekwa ndani yake taa. Taa ile imo katika tungi. Tungi lile ni kama nyota inayo meremeta, inayo washwa kwa mafuta yanayo toka katika mti ulio barikiwa, mzaituni. Si wa mashariki wala magharibi. Yanakaribia mafuta yake kung'aa wenyewe ingawa moto haujayagusa - Nuru juu ya Nuru. Mwenyezi Mungu humwongoa kwenye Nuru yake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.