IQNA

Jinai za Israel

Utawala wa Israel wazidisha mashambulizi Gaza, wapuuza Azimio la Umoja wa Mataifa

10:33 - October 28, 2023
Habari ID: 3477800
TEHRAN (IQNA)- Sambamba na kuanza operesheni ndogo ya nchi kavu ya jeshi katili la utawala haramu Israel kwa lengo la kujipenyeza Ghaza usiku wa kuamkia leo, zaidi ya raia 100 Wapalestina wameuawa shahidi huku utawala huo ukilaaniwa kote duniani kwa kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina. Hayo yamejiri huku Umoja wa Mataifa ukitaka vita visitishwe mara moja.

idadi ya mashahidi wa Kipalestina imeongezeka tangu kuanza kwa mashambulizi ya anga ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza. Utawala haramu wa Israel umevuriga na kuzima intaneti ya Ghaza ili kujaribu kuzuia habari za jinai zake kuwafikia walimwengu..

Duru za Palestina za Palestina zimedokeza, tangu utawala katili wa Israel uanzishe vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ghaza, zaidi ya Wapalestina 7,400 wameuawa shahidi wakati wa mashambulizi hayo na wengine 18,000 wamejeruhiwa.

Aidha vyombo vya habari vya Palestina, katika shambulio la angani la jeshi katili la Israel  jengo la makazi la Hayi al-Shati magharibi mwa Mji wa Ghaza, ambalo lilikuwa makazi ya wakimbizi, zaidi ya raia Wapalestina wapatao 100 waliuawa shahidi.

Jana usiku, vikosi vya Israel vilijaribu kuingia katika mipaka ya mashariki ya ukanda wa Ghaza ambapo vilikumbana na wapiganaji shupavu wa harakati za kupigani ukombozi wa Palestina. Makomando wa  wa utawala wa Kizayuni wa Israel walifeli katika jitihada zao za kujipenyeza ndani ya Ghaza.

Ripoti zaidi zinaonyesha kuwa utawala haramu wa Israel umetumia bomu nyeupe ya fosforasi kaktika mashambulio yake ya jana dhidi ya Wapalestina. Utumizi wa mabomu ya fosforasi karibu na maeneo yenye raia wengi au dhidi ya raia ni jinai ya kivita kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Baraza Kuu UN lapitisha azimio la kulinda raia Ghaza, usitishwaji vita, Israel yapinga

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa llimepiga kura kupitisha azimio la kulinda raia wakati huu ambapo utawala haramu wa Israel umeshadidisha hujuma dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza. Azimio hilo limepitishwa katika kikao cha 10 cha dharura ambacho kimefanyika Ijumaa kwa siku ya pili huku kukiwa na mvutano kwenye Baraza la Usalama na hali katika eneo linalozingirwa la Ghaza ikizidi kuwa mbaya.

Israeli Regime Intensifies Gaza Attacks Despite UN Resolution

Azimio hilo linataka suluhisho la haraka, la kudumu na endelevu la kibinadamu. Azimio hilo ambalo lilipendekezwa na  Jordan limepitishwa na Baraza Kuu, kwa kura 120 za ndio, 14 za kupinga na nchi 45 zilijuzuia kupiga kura.

Katika Baraza Kuu nchi wanachama 193 kila moja ina kura moja, na tofauti na Baraza la Usalama, hakuna kura ya turufu. Maamuzi ya Baraza Kuu kuhusu masuala muhimu hufanywa na theluthi mbili ya wajumbe waliopo na kupiga kura. Utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukiendesha vita dhidi ya Gaza tangu tarehe 7 Oktoba, wakati harakati za muqawama za kupigania ukombozi wa Palestina, Hamas na Jihad Islami zilipoanzisha operesheni yao kubwa zaidi kama jibu kwa jinai za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Idadi ya waliouawa Gaza tangu kuanza kwa uvamizi wa utawala dhalimu wa Israel imefikia zaidi ya 7,400 huku zaidi ya 20,500 wakijeruhiwa.

Kura hiyo katika Baraza Kuu ilikuja baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kushindwa mara nne katika wiki mbili zilizopita kuchukua hatua kutokana na Marekani kupiga kura ya turufu mara kwa mara dhidi ya maazimio dhidi ya Israel.

Viongozi wa Hamas na Mamlaka ya Ndani ya Palestina walikaribisha azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kutaka litekelezwe mara moja.

Haya yanajiri wakati ambao utawala haramu wa Israel umekataa miito yote ya kusitishwa kwa mapigano, ikidai kuwa itanufaisha Hamas.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pia limeutaka utawala wa Israel kubatilisha amri yake ya kuwataka raia wa Gaza kuhamia kusini mwa eneo hilo.

Utawala dhalimu wa Israel uliamuru takriban watu milioni 1.1 huko Gaza, karibu nusu ya wakazi wote wa eneo hilo lililozingirwa, kuhamia kusini mnamo Oktoba 12, kabla ya kuanza uvamizi wa ardhini dhidi ya eneo la pwani.

3485761

 

captcha