IQNA

Fatwa

Dar ul-Ifta ya Misri: Haijuzu Kuipa Misikiti jina la Al-Aqsa

15:24 - November 28, 2023
Habari ID: 3477955
CAIRO (IQNA) – Taasisi ya Dar ul Ifta ya Misri imetangaza kuwa hairuhusiwi au haijuzu kidini kuupa msikiti wowote jina la Al-Aqsa.

Dar al-Ifta, taasisi ya kitaalamu ya kutoa Fatwa, ilitoa kauli hiyo kwa kujibu Istifta (swali). Watu kadhaa walikuwa wameuliza maoni ya Dar ul-Ifta  kuhusu iwapo inakubalika kidini kuupa msikiti jina la Al-Aqsa.

Waliouliza walisema kuna msikiti katika kijiji kimoja cha nchi isiyo ya Kiarabu ambao unajulikana kama Masjid al Aqsa jambo ambalo limeibua hitilafu miongoni mwa watu wa nchi hiyo.

Dar ul-Ifta imesema katika majibu yake kwamba, Msikiti wa Al-Aqsa katika mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem) ni sehemu maalum takatifu yenye hadhi maalum katika Uislamu.

Fatwa hiyo imenukuu Aya ya 1 ya Surah Al-Isra ya Qur'ani  Tukufu isemayo: “ SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu (wa Makka) mpaka Msikiti wa Mbali (Al Aqsa) ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.”

Dar ul-Ifta imeongeza kuwa kutokana na hadhi ya juu ya Msikiti wa Al-Aqsa, kuupa jina msikiti mwingine wowote duniani Al-Aqsa hairuhusiwi kwa mujibu wa mafundisho ya dini tukufu ya Kiisalmu.

4184252

captcha