Kongamano hilo limefanyika katika Haram Takatifu ya Imam Khomeini MA kusini mwa Tehran na kuhudhuria na mjukuu wa Imam Khomeini, Hujjatul Islam Sayyed Hassan Khomeini, mshauri maalumu wa rais wa Iran katika masuala ya kaumu na dini za waliowachache Hujjatul Islam Ali Younesi, balozi wa Syria nchini Iran Shafiq Dayoub pamoja na wanazuoni na wawawakilishi wa harakati za mapambano ya Kiislamu.