IQNA

Algeria yataka wachezaji wake wapewe nakala za Qur’ani Kombe la Dunia

22:15 - April 26, 2014
Habari ID: 1399941
Algeria imetaka waandalizi wa Kombe la Soka la Dunia 2014 kuwapa nakala za Qur’ani wachezaji na maafisa wa timu yake ya taifa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, ikiwa imesalia chini ya miezi miwili kabla ya Kombe la Soka la Dunia la FIFA kuanza nchini Brazil, gazeti moja la Brazil limeripoti kuhusu matakwa ya baadhi ya nchi zinazoshiriki katika mashindano hayo.
Algeria imetaka nakala za Qur’ani ziwekwe katika vyumba vyote vya wachezaji na maafisa wa timu yake. Algeria ni nchi ya Kiislamu iliyo katika eneo la Afrika Kaskazini ambapo karibu asilimia 99 ya wakaazi wake ni Waislamu.
Wakati huo huo Ufaransa nayo imetaka chakula halali cha Kiislamu katika hoteli ambayo watakaa wachezaji na maafisa wa timu yake ya taifa. Ombi hilo la Ufaransa limetokana na kuwa kuna wachezaji kadhaa Waislamu katika timu hiyo ya Ulaya Magharibi.
Kombe la Dunia la FIFA 2014 linatazamiwa kufunguliwa kwa sherehe rasmi Juni 12 ambapo mechi ya ufunguzi itakiwa baina ya Brazil na Croatia Ijumaa Juni 13.

1399503

Kishikizo: algeria soka qur'ani dunia
captcha