IQNA

Wanamichezo Waislamu

Mwanasoka maarufu wa Ufaransa Karim Benzema atunukiwa Qur'ani Tukufu

11:35 - August 18, 2023
Habari ID: 3477455
RIYADH (IQNA) - Karim Mostafa Benzema, mwanasoka wa kulipwa wa Ufaransa ambaye anacheza kama mshambuliaji katika Klabu ya Al-Ittihad ya Ligi Kuu ya Saudia , alipokea zawadi ya nakala ya Qur'ani Tukufu kutoka kwa ripota wa Saudi.

Ibhrahim al-Farian alitoa zawadi hiyo ya Msahafu, ambao pia una tafsiri ya kwa lugha ya Kifaransa, tovuti ya New Misr iliripoti.

Al-Farian alisambaza klipu katika akaunti yake ya kijamii ya X, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter, ambayo inamwonyesha akimpa mchezaji huyo wa Ufaransa zawadi hiyo ya Msahafu.

Karim Benzema ni mmoja wa Waislamu wanaojulikana sana katika ulimwengu wa michezo.

Baada ya kujiunga na Al Ittihad, alikwenda katika mji mtakatifu wa Makka kutekeleza ibada ya Hija ndogo ya Umrah mapema mwezi huu.

Alisambaza mtandaoni klipu hiyo akiwa katika Umrah hukua akiwa amevalia vazi  maalumu la ibada hiyo linalojulikana kama Ihram.

4163093

Habari zinazohusiana
captcha