TEHRAN (IQNA) – Siku kuu ya Idul Fitr ni kati ya siku kuu muhimu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu na kawaida huwa siku ya mapumziko. Mwaka huu katika aghalabu ya nchi za Kiislamu kumekuwa na hali maalumu ya tahadhari wakati wa Idi ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.
Jumapili Mei 2020 ilisadifiana na tarehe Mosi Shawwal mwaka 1441 Hijri na hivyo ilikuwa siku kuu ya Idul Fitr katika aghalabu ya nchi duniani baada ya kumalizika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.