IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu zakithiri Ufaransa, mwanasiasa ataka marufuku ya Hijabu

16:25 - January 30, 2021
Habari ID: 3473604
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi maarufu wa upinzani wa mrengo wa kulia wenye kufurutu ada nchini Ufaransa, Marine Le Pen amependekeza kuwa vazi la Kiislamu la Hijabu lipigwe marufuku kabisa katika maeneo yote ya umma nchini humo.

Kauli hiyo imeathminiwa kuwa ni kushindana na Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo katika sera za chuki dhidi ya Uislamu. Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni, Bi. Le Pen anakaribiana na Macron na hivyo kuna uwezekano akatwaa uongozi nchini huo siku za usoni.

Le Pen amaamua kurejea katika wigo wa kampeni kwa kuibua kadhia ya Hijabu ikiwa imesalia miezi 15 kabla ya uchaguzi mkuu mwakani. Akizungumza na waandishi habari, Le Pen amesema anautazama mtandio na Hijabu kuwa vazi la Kiislamu ambalo linapaswa kupigwa marufuku. Aidha amewasilisha pendekezo la kupigwa marufuku kile alichokitaja kuwa ni 'idiolojia za Kiislamu' ambazo amezitaja kuwa za 'kidikteta' na 'mauaji'.

Tokea achukue hatamu za uongozi wa chama hicho kutoka kwa baba yake, Le Pen amegomea urais wa Ufaransa mara mbili bila mafanikio. Lakini uchunguzi wa maoni unaonyeha kuwa ampata umashuhuri kutokana na sera zake dhidi ya Waislamu, dhidi ya wahamiaji na dhidi ya Umoja wa Ulaya.

Hivi karibuni  kamati maalumu ya Bunge la Kitaifa la Ufaransa iliidhinisha sheria ya 'thamani za jamhuri' ambazo zilipendekezwa na rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo kwa ajili ya kukabiliana na kile alichokitaja ni 'Uislamu wa wanaotaka kujitenga.'

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin amedai katika ukurasa wake wa Twitter kuwa sheria hiyo inalenga kulinda thamani za jamhuri sasa na siku za usoni.

Jumuiya ya Waislamu Ufaransa (CFCM) imepinga vikali sheria hiyo na kuitaja kuwa yenye kuwawekea Waislamu vizingiti katika maisha yao yote.

Sheria hiyo inaipa serikali haki ya kuingilia mambo ya misikiti na kupeleleleza kamati zinazosimamia misikiti na pia kudhibiti matumizi ya pesa za misikiti na asasi za Waislamu.

3473840

captcha