IQNA

Wazayuni waendeleza hujuma dhidi ya Msikiti wa al Aqsa mjini Quds

22:12 - June 28, 2021
Habari ID: 3474051
TEHRAN (IQNA)- Wazayuni wenye misimamo mikali wameuhujumu tena Msikiti wa al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) leo Jumatatu wakiwa chini ya himaya ya wanajeshi wa utawala haramu wa Israel.

Ripoti zinasema kuwa, makumi ya Wazayuni  mapema leo Jumatatu waliuhujumu Msikiti wa Al Aqsa kupitia lango la Al-Magharebah na kuuvunjia heshima huku askari wa utawala wa Israel waliwazuia Wapalestina kutekeleza ibada Msikitini hapo wakati wa hujuma hiyo.

Walowezi hao wa Kizayuni walitekeleza ibada za Kiyahudi katika uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa kabla ya kuondoka wakipitia mlango wa Al Silsila.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

3475084

captcha