IQNA

#for_martyrs' sake

Kampeni ya Kimataifa ya kuwasomea Qur'ani Tukufu mashahidi yazinduliwa

20:30 - December 28, 2021
Habari ID: 3474735
TEHRAN (IQNA)- Kampeni ya Kimataifa ya kusoma Qur'ani Tukufu kwa munasaba wa mwaka wa pili tokea auawe shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani imezinduliwa.

Kampeni hiiyo iliyo na hashtegi ya #for_martyrs' sake itawashirikisha Waislamu kote duniani na imeandaliwa na Taasisi ya Kiutamaduni ya Anwar Rasool Aadham SAW.

Wale wote wanaotaka kushiriki katika kampeni hii wanaweza kusoma aya za mwisho za Sura Al Fajr na kutuma klipu yao ya video katika mitandao ya kijamii kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa,

Hapa chini ni bango la kampeni hiyo.

#For_Martyrs Online Quranic Campaign Launched

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. Hujuma hiyo ya kigaidi ilitekelezwa kufuatia amri ya rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump.

4024296

captcha