IQNA

Rais wa Venezuela: Jamii ya kimataifa ilaani mauaji ya Jenerali Soleimani

20:04 - December 29, 2021
Habari ID: 3474738
TEHRAN (IQNA)- Rais Nicholas Maduro wa Venezuela amesema jamii ya kimataifa inapaswa kulaani vikali mauaji ya kigaidi ya mwaka 2020 ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani wa Iran ambaye alikuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi.

Akizungumza katika mahojiano na televisheni ya Al Mayadeen ya Lebanon, Maduro amelaani mauaji ya Soleimani yaliyofanywa na Marekani na kuyataja kuwa ni jinai ya kuogofya.

Maduro amehoji, "Je hii ndio dunia tunayoitaka, ambayo Ikulu ya White House inatoa amri ya kuuawa shujaa wa vita dhidi ya ugaidi Iraq, Syria na Lebanon?

Maduro amekumbuka namna Shahidi Soleimani alivyotembelea Caracas baina ya Machi na Aprili 2019 na kusema "Jenerali Soleimani alikuwa mwenye tabasamu na matumaini. Namshukuru Mungu kwa kukutana naye,"

 Amesema Shahidi Soleimani alipambana na magaidi na watenda jinai ambao walikuwa wakiwashambulia raia wa kawaida na Mhimili wa Muqawama. "Alikuwa shujaa," amesema Maduro.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. Hujuma hiyo ilitekelezwa kufuatia amri ya rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump.

Rais wa Venezuela pia amesema uhusiano wa nchi yake na Iran ni mzuri na kuongeza kuwa atafika Tehran hivi karibuni kufuatia mwaliko wa Rais Ibrahim Raisi.

Aidha Rais wa Venezuela amesema anamuheshimu Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei na kumtaja kuwa mtu mwenye hekima na busara kubwa.

Akizungumzia zaidi njama za Marekani dhidi ya nchi yake, Rais Maduro ameeleza bayana kwamba, nchi yake itaendelea kupinga na kulaani sera za kibeberu za Washington na washirika wake.

4024059

captcha