IQNA

Kamanda Mkuu wa IRGC

Iran ni nchi ya kwanza ya ulimwengu wa Kiislamu kujirushia satalaiti katika anga za mbali

21:40 - March 08, 2022
Habari ID: 3475023
TEHRAN (IQNA)- Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema kuwa na uwezo wa kujirushia satalaiti katika anga za mbali ni kigezo cha nchi iliyostawi duniani.

Aidha ameongeza kuwa, pamoja na kuwepo vikwazo vingi vya kimataifa, vijana wa taifa la Iran katika IRGC wamefanikiwa kurusha satalaiti katika anga za mbali.

Akizungumza katika hafla ya kurushwa satalaiti ya Nour-2  katika anga za mbali, Meja Jenerali Hossein Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesema satalaiti hiyo imetumwa angani kwa mafanikio wakati huu wa Idi za Mwezi wa Shaaban na kuongeza kuwa: "Ni fahari na jihadi kubwa kuona kuwa, kwa jina la taifa la Waislamu na Mfumo wa Kiislamu, na pamoja na kuwepo vikwazo vingi va kimataifa, vijana wa taifa la Iran katika IRGC, kwa kutegemea imani, irada na ubunifu, wameweza kurusha satalaiti katika anga za mbali.

Kamanda Mkuu wa IRGC amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni nchi ya kwanza ya Kiislamu duniani ambayo imeweza kujirushia satalaiti katika anga za mbali kwa kutgemea wataalamu wake wa ndani ya nchi. Amesema Iran leo imeweza kuwashinda maadui na kumiliki teknolojia muhimu na za kisasa  na kuongeza kuwa, mafanikio hayo yana maana ya kumshinda adui katika vita vya kiktenolojia. Meja Jenerali Salami amesema adui alikuwa anajaribu kuifanya Iran ibaki nyuma kiteknolojia lakini ameshindwa.

4041407

captcha